• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (19 Agosti-25 Agosti)

    (GMT+08:00) 2017-08-25 15:28:59

    Ubalozi wa Marekani nchini Russia kusimamisha utoaji viza

    Ubalozi wa Marekani nchini Russia umesema kuanzia utasimamisha utoaji wa viza zisizo za uhamiaji kote nchini Russia kutokana na kupungua kwa wafanyakazi wake katika ubalozi huo.

    Habari zinasema ubalozi huo mjini Moscow utaanza tena kutoa viza tarehe mosi mwezi ujao, na balozi ndogo mjini St.Petersburg, Ekaterinburg na Vladivostok zinaendelea kusimamisha utoaji viza.

    Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw Sergei Lavrov amesema Russia haitachukua hatua kuwazuia raia wa Marekani kuomba viza ya Russia.

    Wakati huo huo, rais Vladmir Putin amesaini agizo la kumteua Bw Anantoly Antonov kuwa balozi mpya wa Russia nchini Marekani na mwangalizi wa kudumu wa Russia kwenye Muungano wa Nchi za Amerika.

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani umesisitza tena Alhamis kwamba kusimamishwa kwa utoaji viza katika ubalozi wa Marekani nchini Russia kunatokana na kupunguzwa kwa wafanyakazi na sio hatua ya "kulipizia kisasi kwa Russia".

    Mwezi Julai, Russia iliitaka Marekani kupunguza idadi ya wanadiplomasia wake nchini Russia kutoka 755 hadi 455 kabla ya Septemba 1.

    Habari nyingine zinasema Russia haitachukua hatua yoyote kujibu vikwazo vinavyowekwa na Marekani, na itaendelea kutafuta mazungumzo na Marekani.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako