Wanajeshi 99 wa China wa kulinda amani wafunga safari ya kwenda Sudan
Wanajeshi 99 wa China wamewasili nchini Sudan, kufanya kazi za kulinda amani katika sehemu ya Darfur nchini humo. Kabla ya hapo wanajeshi 41 wamesha pelekwa huko Darfur.
Mwaka 2015, rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa alitangaza kuwa, kwa mara ya kwanza, China itatuma kikundi cha wanajeshi 140 wa helikopta kushiriki kwenye kazi za kulinda amani za Umoja wa Mataifa barani Afrika.
Hadi sasa China imewatuma wanajeshi elfu 33 kushiriki kwenye juhudi za Umoja wa Mataifa za kulinda amani duniani kote.
Idadi hiyo ni kubwa zaidi ikilinganishwa na nchi wanachama wengine wanne wa kudumu wa Baraza la Usalama la umoja huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |