Asilimia 92 wapiga kura katika jimbo la wakurd waunga mkono kujitenga na Iraq
Tume ya kura za maoni kuhusu kujitenga kwa jimbo linalojitawala la wakurd imtangaza kuwa matokeo ya mwisho yanaonesha kuwa asilimia 92.73 ya wapiga kura wanaunga mkono jimbo lao kujitenga na Iraq.
Matokeo yalionesha kuwa wapiga kura milioni 2.86 kati ya milioni 3.31 walioshiriki kwenye upigaji kura.
Tume hiyo imesema matokeo rasmi yanapaswa kuidhinishwa na mahakama kuu.
Hata hivyo waziri mkuu wa Iraq Bw. Haider al-Abadi alisisitiza serikali ya mkoa wa Kurdi ifute matokeo ya kura hizo kabla ya kuanza mazungumzo ya kutatua mgogoro.
Serikali ya Iraq kwa nguvu zote inapinga upigaji kura hizo za maoni na inadai kuwa mamlaka ya Kikurdi inapaswa kusalimisha uwanja wa ndege wa Baghdad ama kuwa tayari kukabiliana na hatua za kimataifa dhidi yao
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |