Russia yateketeza silaha zote za kemikali
Serikali ya Russia wiki hi imesema silaha zote za kemikali zimeteketezwa jimboni Volga, kusini magharibi mwa Russia.
Mwenyekiti wa baraza la kupunguza silaha za kemikali Bw Mikhail Babich ameripoti kwa rais Vladimir Putin wa Russia akisema kazi ya kuziteketeza silaha zote za kemikali imemalizika kabla ya wakati uliopangwa.
Rais Putin amesema hili ni tukio kubwa katika historia ya Russia, na ni hatua kubwa kuifanya dunia ya kisasa iwe na uwiano na usalama zaidi. Amesisitiza kuwa Russia umetekeleza kwa makini wajibu wa kimataifa kwenye kupunguza silaha na kuzuia kuenea kwa silaha za nyukllia.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kupiga Marufuku Silaha za Kemikali OPCW Bw Ahmet Uzumucu amesema Russia kuteketeza silaha zote za kemikali kumekuwa hatua muhimu ya kutimiza malengo ya Mkataba wa kupiga marufuku silaha za kemikali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |