Watu 58 wauwawa Las Vegas, Marekani
Zaidi ya watu 58 wameuawa na takriban 515 kujeruhiwa kwenye ufyatuaji wa risasi wakati wa tamasha la muziki huko Las Vegas, Marekani.
Mtu mwenye bunduki mwenye umri wa maika 64 Stephen Paddock alifyatua risasi kutoka ghoroga ya 32 kwenye hoteli ya Mandalay Bay, kwenda kwa tamasha lililokuwa likiendelea nje.
Mamia ya watu walikimbia eneo hilo na milio ya risasi ikasikika kwa muda kwenye video zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii.
Chama cha taifa cha wamiliki wa bunduki Marekani (NRA) sasa kimeonekana kubadilisha msimamo wake na kuunga mkono udhibiti wa vifaa ambavyo hutumiwa kuimarisha uwezo wa bunduki.
Kifaa kama hicho kilitumiwa na Stephen Paddock aliyewaua zaidi ya watu 50 kwenye tamasha hilo la Las Vegas.
Kundi hilo limesema vifaa hivyo huwezesha bunduki ambazo zina uwezo fulani wa kufyatua risasi mfululizo kuwa bunduki kamili za kufyatua risasi mfululizo kwa kujiendesha yenyewe.
Chama cha Republican kimesema kwamba kitajadili uwezekano wa kupiga marufuku kifaa hicho kwa jina 'bump-stock' ambacho huondoa haja ya mtu anayetumia bunduki isiyo na uwezo kamili wa kufyatua risasi mfululizo kutumia bega lake kuidhibiti bunduki wakati wa kufyatua risasi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |