Zaidi ya watu 270 wauwawa kwenye shambulizi Somalia
Zaidi ya watu 270 wameuwawa wiki hii kwenye shambulizi la kigaidi nchini Somaliaa.
kufuatia shambulizi hilo Rais Mohamed Abdullahi Mohamed alitangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kuomboleza waliofariki..
Habari zinasema shambulizi hilo la mabomu yaliyotegwa kwenye lori lilitokea katika barabara iliyoko eneo la kibiashara katikati mwa Mogadishu, yenye majengo ya serikali, hoteli na maduka mengi, na kusababisha msukosuko mkubwa mjini Mogadishu.
Majeruhi 35 walifikishwa mjini Ankara, Uturuki kwa matibabu, na 13 kati yao wamejeruhiwa vibaya. Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na shambulizi hilo.
Shambulizi hilo limelaaniwa vikali na jumuiya ya kimataifa.
Nchini Kenya Mamia ya Wakenya pamoja na raia wa Somalia wanaoishi nchini humo walishiriki katika shughuli ya kutoa damu ili kuwasaidi wale waliojeruhiwa katika mlipuko huo wa bomu.
Kampeni hiyo ya kutoa damu ilizinduliwa kupitia mitandao ya kijamii katika eneo la Eastleigh mjini Nairobi kufuatia bomu hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |