Mwendesha mashtaka wa ICC ahimiza kupelekwa kwa kamanda wa Libya mahakamani
Mahakama ya Kimataifa ya makosa ya Jinai ICC imetoa hati ya kukamatwa kwa Meja Mahmoud al-Werfalli kwa makosa ya kuwaua watu 33 katika mgogoro unaoendelea nchini Libya.
Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo alipotoa hotuba kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, amesema Meja Al-Werfalli ni kamanda wa brigedi ya Al-Saiqa yenye makao makuu huko Benghazi, ambaye amefanya kazi katika "operesheni kwa heshima ya taifa" ya jeshi la taifa la Libya.
Mwendesha mashitaka huyu pia ameihimiza jumuiya ya kimataifa kumkabidhi kiongozi wa zamani wa idara ya usalama wa ndani ya Libya Bw Al-Tuhamy Khaled.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |