Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Priti Patel, ajiuzulu
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Priti Patel, amejiuzulu Jumatano usiku baada ya kukutana na viongozi wa kisiasa wa Israeli bila kujulisha serikali yake.
Priti Patel amekua afisa wa pili kuondoka kwa baraza la mawaziri ndani ya kipindi cha wiki moja, vyanzo vya serikali vimesema.
Priti Patel, mwenye umri wa miaka 45, aliomuomba msamaha Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May na kuomba kujiuzulu na hivyo, kusitisha ziara yake barani Afrika.
Waziri mkuu Theresa May alisema Uingereza na Israeli ni washirika wa karibu na ni sawa kufanya kazi kwa pamoja lakini anafahamu kuwa hilo linapaswa kufanyika kwa njia rasmi, kupitia njia zinazojulikana kiserikali.
Priti Patel amekua waziri wa pili kuacha kazi ndani ya kipindi cha wiki moja baada ya Waziri wa Ulinzi Michael Fallon Novemba 1. Bw. Fallon alihusishwa katika kashfa ya unyanyasaji wa kijinsia inaendelea kuwakabili viongozi wa kisiasa nchini Uingereza na kutishia pia kumfanya ajiuzulu mshirika wa karibu wa Theresa May, Naibu Waziri Mkuu Damian Green, na Waziri wa Biashara ya Kimataifa Mark Garnier.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |