Raia wa Zimbabwe wamekusanyika kwa wingi Ijumaa kwenye uwanja wa michezo katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare kwa ajili ya sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa.
Mnangagwa ameapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla.
Mugabe alikuwa amemfuta kazi Mnangagwa mwezi hali iliopelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke.
Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi".
Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 hapo siku ya Jumanne iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe.
Ilitolewa kwa njia ya barua bungeni na kikao cha kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae kikakatizwa.
Katika barua hiyo Bwana Mugabe alisema anajiuzulu ili kuruhusu mchakato rahisi na wa amani wa ukabidhianaji mamlaka na kwamba uamuzi wake ulikuwa wa hiari.
Alhamis , taarifa zilielezea kuwa Bwana Mugabe amepewa kinga ya kutoshtakiwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |