Palestina yakubali kufanya uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka 2018
Viongozi wa makundi ya wapiganaji na kisiasa nchini Palestina wamekutana na kukubaliana kufanya uchaguzi mkuu nchini humo mwishoni mwa mwaka 2018.
Chama cha Fatah cha rais Mahmoud Abbas na vyama vingine vimesisitiza umuhimu wa kutekeleza kikamilifu maridhiano yaliyofikiwa mwezi Oktoba chini ya usuluhishi wa Misri kati ya chama cha Fatah na kundi la Hamas.
Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo imesema, pande hizo zimeitaka Tume ya Uchaguzi na pande zinazohusika kumaliza maandalizi yanayotakiwa kwa ajili ya uchaguzi wa rais na wabunge ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |