Waziri mkuu wa Somalia awafuta kazi mawaziri watatu
Waziri mkuu wa Somalia Hassan Ali Khaire amewafuta kazi mawaziri watatu katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Habari imesema, mawaziri hao waliofutwa kazi ni pamoja na waziri wa mambo ya nje, waziri wa biashara na viwanda, na waziri wa mambo ya ndani, lakini haikutoa sababu za kufutwa kazi kwa mawaziri hao.
Waziri mkuu huyo pia amemwita nyumbani balozi wa nchi hiyo nchini Marekani Ahmed Isse Awad, kujaza nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje, huku Abdi Mohamed Sabriye akichukua nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani, na Mohamed Abdi Hayir akichukua nafasi ya Waziri wa Viwanda na Biashara.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |