Waziri wa mambo ya nje wa Zambia ajiuzulu
Waziri wa mambo ya nje wa Zambia Bw. Harry Kalaba ametangaza kujiuzulu kutokana na suala la ufisadi kutotatuliwa.
Bw. Kalaba amesema hawezi kuendelea kufanya kazi ndani ya serikali ya Zambia, na kuangalia wenzake wanaotarajiwa kupambana na ufisadi wakiwa mstari wa mbele kwenye uporaji wa raslimali za umma.
Bw. Kalaba amesema amewasilisha barua ya kujiuzulu kwa rais Edgar Lungu, lakini ataendelea kuwa mbunge wa chama tawala cha Zambia.
Katika miezi miwili iliyopita Rais Edgar Lungu amewafuta kazi mawaziri wawili kutokana na tuhuma za ufisadi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |