Serikali ya jimbo la Kurdistan yakamata wapiganaji elfu 4 wa IS
Idara ya usalama ya serikali ya jimbo la Kurdistan imedai kuwa imewakamata wapiganaji wapatao elfu 4 wa kundi la IS, wakiwemo wapiganaji wa nchi za nje wa kundi hilo.
Akitangaza taarifa hiyo, Afisa habari wa serikali hiyo Bw. Dindar Zebari amesema, kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka jana, idara ya usalama na vikosi vya jimbo hilo vimekamata wapiganaji 2,500 wa IS, na kwenye operesheni ya kuukomboa mji wa Hawijah, wapiganaji wengine elfu 1 wamejisalimisha.
Bw. Zebari pia amesema kabla ya hapo wapiganaji 350 wa kundi la IS waliofungwa gerezani mjini Kirkuk wamehamishiwa Erbil.
Ofisa huyo amedokeza kuwa, serikali ya jimbo la Kurdistan imewasilisha orodha ya majina ya wapiganaji hao kwa Umoja wa Mataifa na Kamati ya kimatiafa ya Chama cha Msalaba Mwekundu. Amesema kazi ya kuwakabidhi wapiganaji hao kwa serikali kuu ya Iraq inapaswa kufanyika chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |