• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 3-March 9)

    (GMT+08:00) 2018-03-09 17:45:12

    Museveni amfuta kazi mkuu wa polisi na waziri wa usalama

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amemfuta kazi Inspekta mkuu wa polisi, Kale Kayihura na waziri wa Usalama, Henry Tumukunde.

    Jenerali Kayihura, ambaye ni mkereketwa wa vita vilivyomsaidia rais Museveni kuingia madarakani mwaka 1986, kwa wakati mmoja alikisiwa kuwa afisa mwenye mamlaka makubwa zaidi katika jeshi la Uganda.

    Lakini amekabiliwa na shinikizo kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa usalama.

    Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Uganda yamefurahia kutimuliwa kwa mkuu wa jeshi la Polisi, wakisema jeshi la polisi lilikuwa limeshindwa kulinda usalama wa raia na mali zao wakiongozwa na kinara wao Jenerali Kale Kayihura.

    Zaidi ya wanawake 20 wameuawa katika visa vya mauaji ambavyo havijatatuliwa katika maenoe yanayouzunguka mji mkuu wa Kampala, na katika miezi mitatu iliyopita raia watatu wa kigeni pia wameuawa.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako