Wakimbizi 2,500 wa Burundi nchini DRC wavuka mpaka na kuingia Rwanda
Mamlaka ya mpaka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC imesema, wakimbizi 2,500 wa Burundi kutoka kambi ya mpito iliyoko nchini DRC wamevuka mpaka na kuingia nchini Rwanda.
Ofisa wa Idara ya uhamiaji ya DRC amesema wakimbizi hao waliokuwa katika mji wa Kamanyoka, Kivu Kusini, sasa wapo mjini Bugarama nchini Rwanda.
Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC imetangaza kuwa maofisa wake waliwasindikiza wakimbizi hao hadi mpakani.
Mshauri wa rais Joseph Kabila wa DRC amesema kuwa, Rwanda imekubali kuwapokea wakimbizi hao, na kwamba hao hawakuwa wakimbizi baadhi walikuwa wanaomba hifadhi, lakini maombi yao yalikataliwa kutokana na kushindwa kutimiza baadhi ya matakwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |