Wakimbizi wa Somalia zaidi ya elfu 78 warudi nyumbani kwa hiari kutoka Kenya tangu mwaka 2014
Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR limesema kuanzia mwaka 2014 hadi Machi 15 Mwaka huu, wakimbizi zaidi ya elfu 78 wa Somalia, wengi wao wakiwa wanatoka kwenye kambi ya Dadaab kaskazini mwa Kenya, wamerudishwa nyumbani kwa hiari.
Shirika hilo limesema mwaka huu peke yake wakimbizi zaidi ya elfu 2,900 wamesaidiwa kurudi nyumbani, wengi wao wakienda Kismayu.
Serikali ya Kenya imekuwa ikipanga kufunga kambi ya Dadaab, kutokana na kambi hiyo kuleta changamoto ya kiusalama kwenye mapambano dhidi ya ugaidi.
Hata hivyo ofisi ya UNHCR nchini Somalia iliomba kusitishwa kwa muda kwa kazi ya kurudisha wakimbizi, kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kusababisha barabara kutopitika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |