AU yatoa mafunzo kwa polisi wa Somalia
Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kimeanza wiki hii kutoa mafunzo kwa askari polisi 25 wa Somalia kuwaongezea ujuzi wa kuongoza magari kutokana na ukosefu wa usalama kwenye barabara kadhaa nchini humo.
Kaimu mratibu wa idara ya mafunzo ya polisi na maendeleo ya AMISOM Leon Ngulube amesema, mafunzo hayo ya siku kumi yatawawezesha polisi hao kuwa na ufahamu unaotakiwa, ujuzi na tabia inayotakiwa katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Ngulube amesema polisi wa Umoja wa Afrika wataendelea kujenga uwezo wa jeshi la polisi na maeneo mengine muhimu ili kuwawezesha polisi hao kutimiza wajibu wao katika njia ya kitaalam na kwa kuendana na viwango vya kimataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |