• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai30-Julai 6)

    (GMT+08:00) 2018-07-06 19:10:06

    Nchi wanachama 49 wa Umoja wa Afrika wasaini makubaliano ya biashara huria

    Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Bw. Paul Kagame amesema nchi 49 wanachama wa Umoja huo wamesaini makubaliano ya eneo la biashara huria barani Afrika (AfCFTA).

    Bw. Kagame ambaye pia ni rais wa Rwanda, ametangaza hayo mjini Nouakchott, kwenye ufungaji wa mkutano wa 31 wa kilele wa Umoja wa Afrika. Afrika Kusini, Sierra Leone, Namibia, Lesotho na Burundi zimesaini makubaliano hayo mjiji Nouakchott. Chad na Swaziland zimeidhinisha makubaliano hayo, na kuzifanya nchi zilizoidhinisha makubaliano hayo kufikia 6.

    Eneo la biashara huria la Afrika AfCFTA litakuwa eneo kubwa zaidi la biashara huria tangu shirika la biashara duniani WTO kuanzishwa, na litaisaidia Afrika kuwa na soko la watu zaidi ya bilioni 1.2 lenye pato la GDP la dola za kimarekani trilioni 2.5.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako