China kuwa mwenyekiti wa zamu wa baraza la UM
China itakuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu.
Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu amesema, ikiwa nchi mwenyekiti wa zamu, China itaimarisha utaratibu wa pande mbalimbali na Umoja wa Mataifa, kulinda amani na usalama wa dunia, na kuandaa mikutano miwili ya mjadala wa hadhara inayohusu utaratibu wa pande mbalimbali na operesheni ya kulinda amani barani Afrika.
Bw. Ma pia amesema, pendekezo la China la kuitisha mkutano wa kulinda amani barani Afrika linatarajia kuishawishi jumuiya ya kimataifa kuongeza nguvu na ufuatiliaji katika mambo ya amani na usalama ya Afrika ili kuusaidia Umoja wa Afrika na nchi za Afrika kulinda amani na usalama. Amesema, hivi sasa, hali ya ujumla ya Afrika ni tulivu na kuwa na mwelekeo mzuri, lakini baadhi ya maeneo na nchi bado zinakabiliana na changamoto za mapigano na ugaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |