• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 27-Novemba 2)

    (GMT+08:00) 2018-11-02 19:27:06

    Sudan Kusini yasherehekea makubaliano ya amani

    Sudan Kusini iLisherehekea kusainiwa kwa makubaliano ya mgawanyo wa madaraka yanayolenga kumaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe huku ikitoa wito kwa amani ya kudumu nchini humo.

    Viongozi wa kikanda na kiongozi wa waasi wa nchi hiyo Bw. Riek Machar aliyesaini makubaliano ya amani mwezi wa Septemba na rais Salva Kiir huko Ethiopia, wamejiunga na maelfu ya watu wa nchi hiyo huko Juba kusherehekea makubaliano ya amani, wakati usalama wa mji huo ukiimarika.

    Rais Kiir ametangaza kuwa amewasamehe wapinzaji wake na yuko tayari kusonga mbele ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukomesha mapigano nchini humo. Katika sherehe hizo, Rais Kiir pia ameamuru kuachiwa huru kwa aliyekuwa msemaji wa Machar, Bw. James Gatdet Dak, huku akisema kuwa ingawa Bw. Gatdet amehukumiwa kifo, lakini ataachiwa kutokana na amani.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako