Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Djibout wakutana
Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na mwenzake wa Djibout Mahamoud Ali Youssouf wamekutana leo hapa Beijing.
Bw. Wang Yi amesema, China siku zote inafuatilia kanuni ya usawa katika uhusiano kati yake na Djibout, na kufuata mtizamo sahihi kuhusu maadili na maslahi katika kusaidia Djibout kuharakisha kujiendeleza. Amesema, pande mbili hizo zinapaswa kutumia fursa ya kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika Beijing, na kuhimiza uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya nchi hizo mbili kuendelezwa.
Bw. Youssouf amesema, Djibout itaendeleza uhusiano kati yake na China, na inayakaribisha makampuni mengi zaidi ya China kuwekeza nchini humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |