Waziri Mkuu wa Algeria asema serikali mpya itaundwa hivi karibuni
Maandamano nchini Algeria yanaendelea dhidi ya kuongezwa kwa muhula wa nne wa Abdelaziz Bouteflika.
Hali hiyo inakuja, siku chache baada ya rais Ambdelaziz kutangaza kwamba amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa urais.
Rais wa Algeria alitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu uliokuwa ulipangwa kufanyika Aprili 18.
Waziri Mkuu mpya Noureddine Bedoui ametangaza kwamba serikali mpya itaundwa wiki ijayo.
Noureddine Bedoui ameelezea kwamba serikali itaundwa na watu kutoka tabaka mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vijana, wanawake na mashirika ya kiraia.
Serikali ya Algeria wakati huo huo imesema iko tayari kufanya mazungumzo na upinzani, Naibu Waziri Mkuu Ramtane Lamamra ametangaza Jumatano wiki hii.
Jenerali Ahmed Gaïd Salah, Mkuu majeshi ya Algeria na Naibu Waziri wa Ulinzi, kwa upande wake amebainisha Jumatano kwenye kituo cha televisheni Ennahar kwamba Jeshi la Taifa (ANP) litalinda "katika hali zote "usalama wa nchi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |