Visanduku vyeusi vya ndege ya Ethiopia iliyoanguka vyapelekwa Ufaransa kwa uchunguzi
Shirika la ndege la Ethiopia limetangaza kuwa visanduku vyeusi kutoka kwenye ndege yake aina ya Boeing 737 Max 8 iliyoanguka na kusababisha vifo vya watu 157, vimepelekwa nchini Ufaransa kwa ajili ya uchunguzi.
Uamuzi wa kutuma visanduku hivyo nchini Ufaransa umekuja baada ya mkuu wa Shirika la ndege la Ethiopia Bw. Tweolde Gabremarian, kutangaza kuwa Ethiopia haina vifaa vya lazima kuvifanyia uchunguzi vifaa hivyo. Kabla ya hapo alitangaza kuwa visanduku hivyo vitapelekwa kwenye nchi ya kigeni kwa ajili ya uchunguzi.
Ndege hiyo ilianguka umbali wa kilometa 45 kutoka Addis Ababa dakika chache baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Bole. Baadaye Ethiopia na nchi nyingine nyingi zilitangaza kusimamisha matumizi ya ndege zao aina ya Boeing 737 Max.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |