Kimbunga Idai kimesababisha uharibifu mkubwa katika baadhi ya maeneo nchini Msumbiji, Malawi na Zimbabwe katika kile ambacho Umoja wa mataifa unasema huenda ni janga baya zaidi la hali ya hewa kuwahi kushuhudiwa kusini mwa Afrika.
Mamilioni ya watu walikuwa kwenye njia ya moja kwa moja na kimbunga hicho huku mji wa pwani wa Beira nchini Msumbiji ukiathirika zaidi.
Idadi ya waliyofariki nchini Msumbiji kufikia sasa ni watu 200 lakini rais Filipe Nyusi anahofia idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi.
Maafisa nchini Msumbiji wanasema watu zaidi ya 15,000 wanahitaji kuokelewa haraka na kupewa hifadhi.
Inaarifiwa kuwa watu wengi wamekwama juu ya mapaa ya majengo, na juu ya miti baada ya kupoteza makaazi yao.
Watoa misaada wanasema kuwa mji wa Beira ambao umeharibiwa na kimbuga hicho, kilichosababisha upepo mkali na mafuta, huenda ukawa salama kwa siku mbili au tatu zijazo baada ya maji kuondolewa.
Hasdi sasa idadi ya watu walipoteza maisha nchini Msumbiji ni 300,lakini inahofiwa kuwa huenda idadi ikaongeka.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |