• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 16-March 22)

    (GMT+08:00) 2019-03-22 20:05:10

    New Zealand kupiga marufuku silaha zenye muundo wa kijeshi

    Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amesema nchi hiyo itapiga marufuku silaha za aina yoyote zenye muundo wa kijeshi zilizotumika katika shambulio la mji wa Christchurch,

    Bi Ardern ameeleza kwamba sheria ya kuruhusu marufuku hiyo itaidhinishwa wakati bunge nchini litakapokaa katika wiki ya kwanza ya Aprili.

    Sheria za matumizi ya bunduki nchini humo zimemulikwa tangu mshambuliaji mwenye itikadi kali za ubaguzi wa rangi alipowaua watu 50 katika misikiti miwili Ijumaa iliyopita.

    Bi Ardern amesema ametarajia sheria hiyo mpya kuidhinishwa ifikapo Aprili 11.

    Amesema watu wanaomiliki silaha hizo watasamehewa watakapozisalimisha na pia kutaidhinishwa mpango wa kuzinunua kutoka kwa wamiliki hao , kuruhusu kusalimishwa kwa silaha hizo.

    Bi Ardern amesema maafisa wanakadiria kwamba gharama ya kuzinunua upya silaha hizo kutoka kwa wamiliki huenda ikawa ni "kati ya $100m na $200m.

    Mwanamume huyo aliyejihami kwa bunduki za rashasha ikiwemo ya AR-15, aliwaua waumini waliokuwa katika sala ya Ijumaa. Anaaminika kuikarabati silaha yake kwa kutumia risasi za kiwango cha juu .


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako