Zambia yamaliza zamu yake ya Uenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika
Zambia imemaliza muda wake kama mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, na kueleza kuridhishwa na mchango wake katika Baraza hilo.
Balozi wa Zambia nchini Ethiopia ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu wa nchi hiyo katika Umoja wa Afrika Bi. Susan Sikaneta amesema, Zambia imemaliza muda wake wa miaka mitatu ulioanza mwaka 2016, na kuacha nafasi hiyo kwa Lesotho.
Bi. Sikaneta amesema Zambia ilitumia nafasi yake kama mwenyekiti kufuatilia masuala kadhaa ikiwemo maendeleo ya Mpango wa Umoja wa Afrika wa Kuondoa Silaha ifikapo mwaka 2020, ambao uliandaliwa mjini Lusaka. Mafanikio mengine makubwa yaliyofikiwa wakati huo pia ni kuhimiza utekelezaji wa "Mwezi wa Msamaha wa Afrika" kwa ajili ya kusalimisha na kukusanya silaha zinazomilikiwa isivyo halali, ambao unaadhimishwa mwezi Septemba kila mwaka.
Wakati huo huo Umoja wa Afrika na Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi NATO wametoa wito wa kuongeza ushirikiano katika kuendesha Vikosi vya Akiba vya Afrika ASF.
Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika imesema maofisa wa pande hizo mbili wametoa wito huo kufuatia mkutano wa Kamishna wa Umoja huo anayeshughulikia Rasilimali Watu, Sayansi na Teknolojia Bibi Sarah Anyang Agbor na kamanda wa majeshi washirika ya mseto na kamanda wa jeshi la majini la Marekani barani Ulaya na Afrika Bw. James G. Foggo III.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |