Serikali ya Ethiopia yasema imewarejesha nyumbani wakimbizi wa ndani 875,000
Polisi katika mkoa wa Benishangul Gumuz uliopo magharibi mwa Ethiopia wamewakamata watu 62 wanaohusishwa na vurugu kali za kikabila.
Polisi wa Mkoa wa Benishangul Gumuz Mohammed Hamednil amesema watu hao 62 walikamatwa wakiwa na mamia ya silaha butu ambazo zinaaminika kwamba watuhumiwa hao walizitumia kwenye mashambulizi hayo ya kikabila. Mapigano hayo yanahusisha kabila la Gumuz na kabila la Amhara.
Habari zaidi zinasema serikali ya Ethiopia katika wiki za karibuni imewarejesha nyumbani wakimbizi wa ndani 875,000 waliokimbia mapambano na vurugu. Kwa mujibu wa msemaji wa serikali Billene Seyoum, serikali pia inashughulikia kuwarejesha wakimbizi waliosalia na kuwafikisha mahakamani wale wanaohusika na msukosuko huo wa wakimbizi wa ndani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |