Wakenya zaidi ya 11 wauawa kwenye mapigano karibu na mpaka kati ya Kenya na Ethiopia
Zaidi ya raia 11 wa Kenya wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea jumatatu kwenye kaunti ya Marsabit, iliyo mpakani kati ya Kenya na Ethiopia.
Ofisa wa serikali ya kaunti hiyo Bw. Mamo Honicha amesema, washambuliaji kutoka Ethiopia waliwapiga risasi wakazi wa huko waliokuwa kwenye mkutano wa kutatua masuala kati ya jamii za jirani.
Kamishna wa wilaya ya Marsabit Bw. Gilbert Kitiyo amesema serikali itachukua hatua ili kutatua mgogoro huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |