Boeing yaboresha mfumo wa ndege 737 Max
Kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing wiki hii ilitoa taarifa ikisema tayari imeboresha mfumo wake ndege ya chapa -737 Max- iliyopigwa marufuku kufuatia ajali zilizosababisha vifo vya abiria wengi katika kipindi cha miezi mitano.
Kampuni hiyo ya Marekani imetangaza kuwa tayari imekwishafanya safari 270 za ndege ya 737 Max yenye programu iliyoboreshwa.
Imeongeza kuwa itatoa taarifa kwa utawala wa safari za anga nchini Marekani-Federal Aviation Administration (FAA) -juu ya namna rubani anavyowasiliana na waongozaji wa ndege na hatua anazopaswa kuchukua kwa matukio mbali mbali. FAA inatarajia Boeing iwasilishe taarifa juu ya namna ilivyoboresha ndege yake kwa ajili ya kupewa idhini ya kupaa tena wiki ijayo.
Ndege ya Ethiopian Airlines ilianguka mwezi Machi na kuwauwa watu wote 157 waliokuwemo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |