Tajiri wa Tanzania amkana mtoto wake kwa usimamizi mbaya wa mali
Si jambo la kawaida, baba anamkana mtoto wake wa kumzaa, na kutangaza kuwa hatahusika tena na mali zake.
Baba aliyetoa tangazo hilo kwenye magazeti nchini Tanzania ni Bw Ramanlal Patel, akimlenga mtoto wake Veer Patel.
Bwana Ramanlal ni mmoja wa wanahisa wakubwa wa Makampuni ya Motisun pamoja na mdogo wake Subhash Patel. Motisun ni moja ya makampuni makubwa na yenye mafaniko Tanzania na ni muunganiko wa makampuni 35. Familia ya Patel ni moja ya familia tajiri zaidi nchini Tanzania.
Katika tangazo ambalo limechapishwa kwenye magazeti siku ya jumatano Bw Ramanlal Patel amesema Januari 31, 2019 alipata notisi ya kutolewa kwenye ukurugenzi wa makampuni hayo. Kwenye notisi hiyo, Bw Ramanlal amedai kuwa, mtoto wake Veer Patel alipata kibali cha mahakama Januari 31 kumpeleka Hospitali ya Taifa ya muhimbili kufanyiwa uchunguzi wa akili. Motisun wanamiliki hoteli maarufu nchini Tanzania za White Sands na Sea Cliff.
Kampuni hiyo pia ndiyo wazalishaji wa juisi na maji chapa ya Sayona, saruji chapa Mamba. Bidhaa nyingine maarufu ni rangi, mabati na matangi ya kuhifadhia maji ya chapa Kiboko.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |