Ethiopia yarudisha wakimbizi milioni 1.2 wa ndani
Waziri wa amani wa Ethiopia Bibi Muferiat Kemal amesema, wakimbizi milioni 1.2 wa ndani wamesaidiwa na kurudi kwenye makazi yao katika miezi michache iliyopita.
Bibi Muferiat pia amesema, Ethiopia inapanga kurudisha wakimbizi wengine milioni 1.1 wa ndani kabla ya mwisho wa mwezi wa Juni, huku serikali ya nchi hiyo ikijitahidi kuhakikisha usalama wa wakimbizi hao watakaporejea kwenye makazi yao.
Habari zinasema, mapema mwezi huu, serikali ya Ethiopia imetangaza kufunga kambi 45 za kupokea wakimbizi hao, ikiwa ni sehemu za juhudi za nchi hiyo kuwarejesha makwao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |