Jeshi la Nigeria layalaumu mashirika ya kibinadamu kwa kulisaidia kundi la Boko Haram
Jeshi la Nigeria limeyatuhumu mashirika ya kibinadamu katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kwa kulisaidia kundi la Boko Haram, na kuonya kuwa linapinga kitendo hicho.
Katika taarifa yake, msemaji wa jeshi hilo Sagir Musa amekataa kutoa majina ya mashirika ya kibinadamu yanayoshukiwa kulipatia kundi hilo misaada kama vile chakula. Hata hivyo, Bw. Musa amethibitisha kuwa mpiganaji wa ngazi ya juu wa kundi hilo amekamatwa wakati akipokea msaada wa chakula kutoka shirika moja la misaada ya kibinadamu lililoko eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambapo kuna mapambano makali dhidi ya magaidi.
Amesema mpiganaji huyo wa Boko Haram aliyetambuliwa kuwa ni Muhammed Modu, alikamatwa na askari jumapili iliyopita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |