Boeing yaahidi kutoa dola milioni 100 kusaidia familia za wahanga wa ajali za ndege nchini Indonesia na Ethiopia
Kampuni ya Boeing imetangaza kutoa dola za kimarekani milioni 100 ili kushughulikia mahitaji ya familia za wahanga wa ajali mbili za ndege aina ya Boeing 737 Max 8 zilizotokea nchini Indonesia na Ethiopia mwezi Oktoba mwaka jana na mwezi Machi mwaka huu.
Mkuu wa Boeing Dennis Muilenburg amesema kampuni yake itashirikiana na serikali za nchi hizo na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa pesa hizo katika miaka kadhaa ijayo.
Wachunguzi wa ajali za ndege wameangazia zaidi mfumo wa kudhibiti ndege hiyo na kampuni ya Boeing imekuwa akishirikiana na wathibiti kuweka mfumo mpya.
Ndege ya Boeing aina ya 737 Max imezuiwa tangu mwezi Machi huku kukiwa hakuna tarehe ya ni lini itaruhusiwa kupaa tena.
Dennis Muilenberg , mwenyekiti na afisa mtendaji wa Boeing alisema katika taarifa yake siku ya Jumatano kwamba kampuni hiyo inaomba radhi kwa maisha yaliopotea katika ajali zote mbili na kwamba maisha yaliopotea yataendelea kuwa mzigo katika mafikra yao kwa miaka kadhaa.
Nomi Husain , wakili anayetoka katika jimbo la Texas nchini Marekani anayewakilisha baadhi ya waathiriwa wa ndege aina ya ET 302 alisema kuwa malipo hayo ya Boeing hayafikii hata kidogo kile ambacho familia za waathiriwa wamepotoza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |