Kenya na Sudan Kusini zakubaliana kutuliza jamii za eneo la mpakani ili kuimarisha amani ya kikanda
Kenya na Sudan Kusini zimekubaliana kutuliza jamii za eneo la mpakani kati ya nchi hizo mbili ili kuhimiza amani ya kikanda.
Gavana wa Kaunti ya Turkana nchini Kenya Bw. Josphat Nanok na Gavana wa jimbo la Kapoeta nchini Sudan Kusini Bw. Louis Lojore wamekutana mjini Nairobi kujadili masuala ya mpaka wa pamoja.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na magavana hao baada ya mkutano inasema, pande hizo zitajitahidi kutatua masuala yoyote kwa njia za kidiplomasia, ikiwemo Programu ya Mpaka ya Umoja wa Afrika, bila uingiliaji wa upande wa tatu.
Habari nyingine zinasema, Kenya na Sudan Kusini pia zinajadili makubaliano ya ushirikiano ili kutatua uhaba mkubwa wa umeme mjini Juba. Chini ya makubaliano hayo, Kenya itatoa umeme wa joto la ardhini kubadilishana na gesi asilia kutoka Sudan Kusini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |