Korea Kaskazini imetaja majaribio ya makombora yake mapya siku ya Alhamisi kuwa onyo rasmi dhidi ya kile ilichokitaja kuwa uchokozi wa Korea Kusini.
Kombora hilo la masafa mafupi lilirushwa katika bahari ya Japan , pia ikijulikana kama bahari ya magharibi kutoka Wonsan katika pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini.
Kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un alisema kuwa taifa lake lililazimika kuunda silaha ili kukabiliana na tishio la moja ka moja.
Amesema kuwa jaribio hilo lilishirikisha mfumo wa kiufundi wa kuelekeza makombora.
Matamshi ya bwana Kim yanajiri baada ya Korea Kaskazini kukosoa uamuzi wa Korea Kusini na Marekani kushiriki katika zoezi la pamoja la kijeshi mwezi ujao.
Korea Kaskazini imetaja zoezi hilo la kijeshi kama maandalizi ya kulivamia taifa hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |