Rais wa Tanzania John Magufuli asafiri kwa Treni kwenda Rufiji
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mara ya kwanza tangu awe rais anasafiri kwa Treni kuelekea Rufiji.
Aliingia kwenye moja ya mabehewa ya treni ya TAZARA kwa ajili ya safari ya kuelekea kuweka jiwe la msingi kwenye mradi mkubwa wa kufua umeme katika mto rufiji utakaozalisha umeme wa kilowati 2115
Watu mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti kuhusu hatua ya rais Magufuli kusafiri kwa Treni badala ya usafiri ambao kwa maoni yao wanaona kuwa unamfaa zaidi kwa hadhi yake, wengine wakiona ni jambo jema na kuwataka viongozi wengine ambao hutumia usafiri wa hadhi ya juu kufuata mfano wa rais Magufuli. Awali kabla ya kupanda treni, Rais Magufuli alizungumza na viongozi wa TAZARA na kuwataka kuwasilisha mapendekezo yao juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuboresha usafirishaji wa mizigo na abiria kupitia TAZARA.Rais Magufuli amesema Serikali inatambua umuhimu wa shirika hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |