Waziri mkuu mpya wa Uingereza ateua baraza lake la mawaziri
Waziri mkuu mpya wa Uingereza Boris Johnson wiki hii aliteua mawaziri wake wa awamu ya mwanzo alhamisi jioni saa chache baada ya kushika wadhifa huo.
Katika kile kinachotajwa kuwa mabadiliko makubwa ya kisiasa tangu mwanzoni mwa miaka ya 1960, zaidi ya nusu ya mawaziri waliokuwa chini ya waziri mkuu wa zamani Bi. Theresa May wameondolewa kwenye nyadhifa zao ama kujiuzulu.
Wakati Johnson akitekeleza hatua hiyo, maelfu ya watu walikusanyika mbele ya jengo la ofisi za waziri mkuu huyo katika Mtaa wa Downing wakipinga uteuzi huo, hatua iliyowalazimu polisi kuweka kizuizi kutowaruhusu waandamanaji hao kuingia kwenye ofisi hizo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |