BokoHaram lasababisha vifo vya raia elfu 27
Mratibu wa mambo ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Nigeria Bw. Edward Kallon amesema, katika miaka 10 iliyopita, kundi lenye msimamo mkali la Boko Haram limesababisha vifo vya raia elfu 27 kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Aliongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, mashirika ya kimataifa ya kibinadamu yakishirikiana na serikali ya Nigeria, yamefungua kambi kwa watu milioni mbili waliopoteza makazi yao, na kutoa misaada ya chakula kwa watu zaidi ya milioni tano.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |