Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan (TMC) Abdel-Fattah Al-Burhan amesema jeshi la Sudan litalinda mpito wa kidemokrasia wa nchi hiyo na kushikilia malengo ya mapinduzi ya Wasudan.
Akihutubia moja kwa moja kupitia televisheni wakati wa kuadhimisha miaka 65 ya kuanzishwa kwa jeshi la Sudan, Bw. Al Burhan amesema jeshi hilo lina uwezo wa kulinda mpito wa kuelekea utawala wa kidemokrasia utakapoanza nchini humo, na litashirikiana na wasudan ili kutimiza ustawi.
TMC na muungano wa upinzani wa Uhuru na Mabadiliko zinatarajiwa kusaini makubaliano ya mwisho kuhusu katiba ya mpito, ambayo itaamua taasisi za utawala katika kipindi cha mpito cha miezi 39.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |