Dawa mpya za Ebola zaonesha ufanisi wa asilimia 90 nchini DRC
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema dawa mbili mpya zilizotumiwa kwa majaribio kwa watu walioambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimeonesha ufanisi wa zaidi ya asilimia 90 kwa wagonjwa waliotumia dawa hizo ndani ya siku tatu baada ya kuonesha dalili za kuambukizwa homa hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Shirika hilo Bw. Christian Lindmeier imesema, eneo la mashariki mwa nchi hiyo bado linakabiliwa na changamoto kubwa baada ya mlipuko wa Ebola nchini DRC kutangazwa kuwa janga la dharura la kiafya la kimataifa mwezi uliopita.
Habari nyingine zinasema kuwa, mamlaka ya usafiri wa anga nchini Nigeria ilitangaza kuwa ndege zote za ndani na za kimataifa zitafuatiliwa kwa kiwango cha juu ili kuzuia virusi vya Ebola kuingia nchini humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |