Ajali yauwa 18 DRC
Watu kumi na nane wamepoteza maisha na wengine ishirini na moja wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika mtaa wa Maluku, inje kidogo na mji wa Kinshasa.
Ajali hiyo imesababiswa na uzembe wa dereva, ambaye alimruhusu msaidizi wake kuendesha gari wakati alikuwa hana uzoefu wa kuendesha gari.
Hata hivyo polisi imesema kuwa idadi ya watu walifariki dunia inaweza kuongezeka, ikibaini kwamba ripoti iliyotolewa ni ya muda.
Gari hilo lililokuwa likisafiri kutoka mji wa Kinshasa kwenda eneo la Nganda Bangala, huku likiabiri watu mia moja, pamoja na bidhaa, lilipinduka na kusababisha vifo vya watu kumi na nane, watu ishirini na moja wamejeruhiwa, kwa mjibu wa Sylvano Kasongo mkuu wa polisi mjini Kinshasa.
Polisi imesema, uzembe wa dereva ndiyo chanzo cha ajali hiyo, baada ya kuona amechoka na safari ndefu, aliamua kumruhusu msaidizi wake kuendesha gari wakata alikuwa hana uzoefu wa kuendesha gari inayosheheni mizigo.
Wakazi wa eneo hilo wameshtumu polisi kuchelewa kuokowa watu kutokana na ukosefu wa vifaa maalumu.
Mashahidi wanasema abiria wengi walifariki kwa kukosa usaidizi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |