Kundi la wadukuzi lakamatwa Rwanda
Kundi la wadukuzi kutoka nchi za Afrika mashariki limetiwa nguvuni nchini Rwanda lilipokuwa likijaribu kuingilia mifumo ya benki.
Idara ya upelelezi nchini Rwanda ilisema wadukuzi hao walipanga kuiba pesa kutoka kwenye akaunti ya mteja wa benki ya Equity, lakini haikusema ni lini jaribio hilo lilifanyika. Ofisi hiyo imesema kuwa kundi hilo linawajumuisha Wakenya wanane, Wanyarwanda watatu na Mganda mmoja. Benki ya Equity Bank ni moja ya benki kubwa katika kanda ya Afrika mashariki na kati ikiwa na matawi yake katika mataifa ya Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Sudan Kusini na Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo.
Idara ya upelelezi ya Rwanda imesema kuwa awali kundi hilo lilifanikiwa kuingilia mifumo ya benki hiyo katika nchi za Kenya na Uganda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |