Wanaharakati wamtaka Imran Khan ajiuzulu
Maelfu ya wanaharakati kutoka vyama vya upinzani vya Pakistan wamepiga kambi katika mji mkuu wa nchi hiyo- Islamabad katika juhudi za kumlazimisha waziri mkuu Imran Khan kujiuzulu. Maandamano hayo yaliongozwa na kiongozi wa kiislamu Maulana Fazlur Rehman na wengi wa waandamanaji ni kutoka chama chake cha siasa za mrengo wa kulia cha Jamiat Ulama-e-Islam. Rehman alianza maandamano hayo na wafuasi wake kutoka mji wa Kusini wa Karachi siku ya Jumapili na kutembea takriban kilomita elfu 2 kufika Islamabad usiku wa manane Alhamisi. Makundi mengine ya upinzani ikiwa ni pamoja na la aliyekuwa rais, Asif Ali Zardari na aliyekuwa waziri mkuu Nawaz Sharif pia yalijiunga na maandamano hayo na kuongeza shinikizo dhidi ya waziri mkuu Khan.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |