Watu 15 wafariki baada ya ndege kuanguka
Watu 15 walifariki dunia siku ya ijumaa baada ya ndege iliyokuwa imewabeba abiria 98 na wafanyakazi kuanguka nchini Kazakhstan. Kwa mujibu wa maafisa wa uwanja wa ndege wa nchi hiyo, ndege hiyo ya Bek Air ilianguka muda mfupi baada ya kupaa katika uwanja wa Almaty mapema siku ya Ijumaa.
Watu 35, wakiwemo watoto wanane walipelekwa hospitali. Ndege hiyo ni ya aina ya FlightZ92100.
Habari zinasema kulikuwa na hali mbaya ya hewa huku kukiwa na ukungu mzito katika eneo la mkasa ijapokuwa bado haijulikani ni nini kilichosababisha ajali hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa ikielekea katika mji mkuu wa Kazakhstan wa Nursultan kutoka mji mkubwa wa Almaty. Inadaiwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa moja na dakika 22 , kabla ya kugonga kizuizi kimoja na kuangukia nyumba ya ghorofa mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |