Mapambano kati ya wafanya biashara na waasi yasababisha vifo vya watu 40
Watu 40 wameuawa kwenye mapambano kati ya wamiliki wa biashara na makundi ya waasi yaliyotokea huko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu usiku wa Krismasi.
Mapambano hayo yalitokea kwenye kituo kimoja cha biashara huko Bangui ambako pia ngome ya makundi ya waasi. Wakazi wa huko wamesema waasi walidai kodi kutoka kwa wamiliki wa biashara wanaouza vitu vya Krismasi, na kupelekea ugomvi uliosababisha mapigano ya kisilaha kati ya pande hizo mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |