Papa Francis aomba radhi kwa kukosa uvumilivu usiku wa mwaka mpya baada ya kumchapa kofi mwanamke
Papa Francis ameomba radhi kwa kitendo chake cha kumchapa kofi, mmoja wa waumini kwenye kanisa la St Peter's Square huko Rome. Papa alikuwa akisalimiana na watoto na mahujaji na wakati akigeuka mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye umati wa watu waliokuwa karibu aliuvuta mkono wa Papa kwa nguvu karibu amuangushe.
Hali iliyomfanya Papa kugeuka na kumpiga makofi mawili mkononi mwanamke huyo kwa hasira. Badaye Papa alikiri kwamba alishindwa kujizuia na yeye pia huwa anakosea kama binadamu wengine. Hivyo anaomba radhi kwa kitendo hicho kwa muumini huyo na kila mtu.
Kitendo cha Papa cha kumzaba makofi ya mkononi mwanamke huyo, kimezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, hasa Twitter, wengi wakimuunga mkono Papa. Awali wakati wa hotuba yake ya mwaka mpya, Papa alikemea unyanyasaji dhidi ya wanawake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |