Mazungumzo ya pande tatu kuhusu GERD kwenye mto Nile kuendelea
Misri imetangaza kuwa mazungumzo ya pande tatu yanayopatanishwa na Marekani kuhusu bwawa la GERD kwenye mto wa Nile bado yanaendelea. Mkutano huo uliofunguliwa Januari 28 ulipangwa kufungwa Januari 29 na kufikia makubaliano ya pande zote. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Misri Bw. Ahmed Hafez amesema, waziri wa mambo ya nje na waziri wa maji wa nchi hiyo wamehudhuria mkutano huo uliofanyika huko Washington, ambapo Misri, Sudan na Ethiopia zinajadili masuala ya bwawa hilo. Ameongeza kuwa mjumbe wa Benki ya Dunia pia amehudhuria mkutano huo ili kufikia makubaliano ya pande zote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |