• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • :Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 8-February 14)

    (GMT+08:00) 2020-02-14 19:47:01

    Rungu la Moi sasa launganisha 'vitoto vya kifalme' nchini

    KUTEULIWA kwa Seneta wa Baringo, Gedion Moi kumrithi kisiasa baba yake Daniel Moi, na kauli ya ndugu yake Raymond kumtaka ashirikiane na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga, kumefufua mjadala wa watatu hao waliozaliwa katika familia tajiri na zenye ushawishi kuendelea kuteka siasa za Kenya.

    Wakati wa mazishi ya Mzee Moi eneo la Kabarak mnamo Jumatano, Bw Raymod Moi alitangaza kuwa familia ya baba yake, aliyekuwa rais wa pili wa Kenya, imemteua Gedion kuwa msemaji wake katika masuala ya kisiasa.

    Alimtaka aimarishe chama cha Kanu na kukitumia kuunganisha Wakenya wote. nyuma ya Rais Kenyatta na Bw Odinga.

    Gedion, kitinda mimba wa hayati Moi, alikubali wadhifa huo na atajiunga na Rais Uhuru ambaye ni msemaji wa familia ya Jomo Kenyatta aliyekuwa rais wa kwanza wa Kenya, na Raila mwana wa aliyekuwa makamu wa rais wa kwanza wa Kenya, Jaramogi Oginga Odinga.

    Wadadisi wanasema hii inaashiria kujiri kwa muungano mkubwa wa kisiasa unaoshirikisha familia za Moi, Odinga na Kenyatta.

    Bw Odinga ndiye kigogo wa kisiasa eneo la Nyanza, wadhifa aliorithi kutoka kwa baba yake, naye Uhuru ndiye msemaji wa eneo la Mlima Kenya ambalo baba yake alimiliki kwa miaka mingi hadi kifo chake. Kwa miaka mingi, Daniel Moi alikuwa kigogo wa siasa eneo la Rift Valley.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako