Baada ya Cardi B kusema ataomba uraia wa Nigeria Lil Wayne naye atangaza kuwa na asili ya taifa hilo
Baada ya Cardi B kusema ataomba uraia wa Nigeria Lil Wayne naye atangaza kuwa na asili ya taifa hilo
Rapa na raia wa Marekani Lil Wayne amekonga nyoyo za raia wa Nigeria baada ya kutangaza kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa vina saba vyake amebaini rasmi kuwa asilimia 53 ya asili yake ni Nigeria."Asili yangu ni Nigeria kuliko Marekani" Lil Wayne.
Hivi sasa raia wengi hasa wa mataifa ya ughaibuni wamekuwa wakipima kipimo hicho maalumu ili kujua asili zao.
Sakata la Lil Wayne kwenda nchini Nigeria inakuja baada ya nyota wengine wa muziki kutoka Marekani kama Cardi B, Meghan Thee Stallion ambaye alifanya Ziara au tour mwezi Desemba 2019 katika nchi za Afrika Magharibi.
Hii ya Cardi B ilitokea mwezi January ambayo ilitokana na machafuko yaliyokuywa yakiendelea nchini Iran baada ya Jenerali wa taifa hilo kuuliwa Qasem Soleimani huko katika mji wa Baghdad nchini Iraq wakati anatoka katika uwanja wa ndege.
Rais wa Marekani Donald Trump alisema kuwa yeye haogopi na endapo Iran wataleta chokochoko basi hatasita kuwashambulia kwani taifa lake la Marekani lina silaha za kutosha na za gharama sana.
Kutokana na kauli hiyo baadhi ya wasanii kutoka Marekani wameonyeshwa kukerwa na kauli hiyo ya Trump na badala yake wameanza kutangaza kutafuta urai wa nchini mbili yaani kutafuta urai wa baadhi ya mataifa ya Afrika.
Miongoni mwa wasanii hao ni Rapper wa kike mwanadada Belcalis Marlenis Almánzar alimaarufu Cardi B ambaye ametangaza kuhamia nchini Nigeria na kuongeza kuwa ataendelea kuwashawishi baadhi ya wasanii wenzake kuhama Mareknai.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |