Askari 33 wa Uturuki wanadaiwa kuuwawa katika mashambulio ya anga ya "vikosi vya Syria" Kaskazini-Magharibi mwa Syria.
Gavana wa jimbo la Uturuki la Hatay Rahmi Dogan amenukuliwa akisema kuwa wengi waliumizwa katika jimbo la Idlib huku idadi ya vifo ikisemekana kuwa juu zaidi.
Uturuki kwa sasa inajibu kwa kushambulia maeneo ya vikosi vya Syria.
Vikosi vya Syria vinavyoungwa mkono na Urusi vinajaribu kurejesha jimbo la Idlib ambalo kwa sasa linadhibitiwa na waasi wanaosaidiwa na wanajeshi wa Uturuki.
Hadi sasa Syria haijatoa kauli yao wazi kuhusu mapigano ya sasa ya Idlib, likiwa jimbo la mwisho lililosalia mikononi mwa upinzani.
Jeshi la Uturuki lilianza kupiga maeneo ya Syria baada ya Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan kufanya mkutano na maafisa wa ngazi ya juu wa usalama mjini Ankara.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |